Kila Linalotokea Maishani Mwako Mhusika Mkuu ni Wewe Mwenyewe

Mpendwa rafiki yangu karibu tena katika makala ya leo ambayo bado inajikita kwenye nguvu ya kubadili fikra na mtazamo wako katika maisha yako ya kila siku hasa katika kuelekea kwenye utajiri. Katika makala zilizopita tumeona jinsi ambavyo unaweza kuamua kuwa tajiri kwa kubadili fikra zako. Naamini unaendelea kufanyia kazi maarifa uliyoyapata kutoka kwenye makala zilizotangulia ili baada ya muda tuweze kusherekea pamoja mafanikio ya kubadili nchi hii kuwa mahala pazuri pa kuishi. 

Katika makala ya leo tutaangalia jinsi ambavyo katika maisha watu wengi wameshindwa kufikia malengo yao kwa vile wamekuwa wakijiona kama si wahusika wakuu kwa kila jambo linalotokea maishani mwao. Tabia hii imepelekea wahusika hawa kuwa walalamikaji pale mambo yanapokwenda kinyume na matarajio. Wakati mwingine mtu anaanza kulalamika hata kabla hajajaribu kufanya kile ambacho anaamini kingemtoa kimaisha.

Epuka kuwa mlalamikaji
Kwanza fikiria juu ya mafanikio ambayo umeweza kuyapata mpaka sasa katika nyanja mbalimbali na pili jiulize ni mikakatij/jitihada zipi ulizojiwekea wewe mwenyewe ili kufanikisha manikio hayo. Ni dhaihiri kuwa sehemu kubwa ya ushindi wako inatokana na mikakati unayojiwekea mwenyewe pasipo kumtegemea mtu. Kwa maana hiyo hakuna atakayekuja kukuambia kuwa muda umefika wa wewe kutimiza ndoto zako hisipokuwa wewe mwenyewe ndo mwenye jukumu la kuhakikisha unatimiza ndoto moja baada ya nyingine.

Katika kufanikisha hili inahitajika nidhamu ya hali ya juu kuhakikisha kuwa wewe unajiona kuwa ni meneja wa maisha yako mwenyewe ili pale mambo yasipoenda sawa uwe wa kwanza kujisuta mwenyewe. Siri kubwa iliyopo hapa ni kuwa pale unapokuwa mlalamikaji hali hii inakufanya ujitoe katika mbio za mapambano hivyo kupelekea kusubilia muhujiza ujitokeze ili kutimiza malengo yako. Kuanzia leo hii jione kuwa hakuna mtu au taasisi yoyote ile inayohusika kwa njia yoyote ile katika kuwezesha kutimiza ndoto zako bali ni wewe mwenyewe (no one to blame except yourself). Suala la ulalamikaji husilipe tena nafasi kwani itakuwa sawa na kujilalamikia mwenyewe kwamba umeshindwa kutimiza wajibu wako.


Mafanikio ni mchakato
 Mafanikio yanapatikana kwa mchakato maalamu wenye malengo mahususi ambayo ni lazima uyafanyie kazi katika maisha yako ya kila siku. Katika kutimiza ili naomba utambue kuwa mafanikio yanapatikana kwa kufuata kanuni ndogondogo ulizojiwekea kwa kipindi cha muda maalumu uliojiwekea pasipo kuvunja kanuni hizo (success is created by following simple fundamental principles consistently overtime). Kutokana na maana hii, mafanikio ya kesho yanatokana na kile unachokifanya kwa sasa katika kila siku ya maisha yako.

Kama utatimiza kanuni ambazo umejiwekea itakufanya uweze kuuona ushindi katika kila iitwapo leo. Ninachomaanisha hapa ni kwamba kanuni utakazojiwekea ili zikuwezeshe kupata utajiri kanuni hizo ni sawa na ngazi ambazo kila siku utakuwa unapanda kutoka ngazi moja hadi nyingine. Kwa hali hiyo itakuwa rahisi kwako kuona jinsi unavyopiga hatua tofauti na pale ambapo husingekuwa na kanuni zozote zinazokuongoza. Kinyume chake ni kwamba mtu ambae hana kanuni zinazomuongoza ni rahisi kukata tamaa kwa sababu atakuwa anadhani kuwa mafanikio ni suala la siku moja.

Hitimisho
Fikiria leo hii unafanya nini ambacho kinaweza kuwa msingi wa mafanikio yako kwa siku zijazo. Fikiria umejiwekea kanuni zipi ambazo zitakusaidia kutimiza ndoto zako kwa muda ujao. Fikiria mpaka sasa umepoteza fursa zipi kwa sababu tu ya kujiona kuwa mazingira hayaridhishi jambo lilopelekea uanze kulalamikia jamii inayokuzunguka au serikali. Mwisho malizia kwa kujisemea kuwa wewe ndo muhusika wa maisha yako na pale utakaposhindwa kutimiza ndoto zako jisemee mwenyewe kuwa umeshindwa kwa uzembe wako.

Kaulimbiu yangu……“FIKRI NA UCHAGUE UTAJIRI KWA KILA ULIFANYALO”

Imeandaliwa na Ndg. Augustine M. Bilondwa
Karibu kwenye fikra za kitajiri  tubadilishane mawazo kupitia mawasiliano yafuatayo:-
Namba ya Simu ya Mkononi                            0786 – 881155/0763 – 745451
Barua pepe                                                    bilondwam@yahoo.com

Blog                                                             fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(