Mpendwa rafiki yangu karibu tena katika
makala ya leo ambayo bado inajikita kwenye nguvu ya kubadili fikra na mtazamo
wako katika maisha yako ya kila siku hasa katika kuelekea kwenye utajiri. Katika
makala zilizopita tumeona jinsi ambavyo unaweza kuamua kuwa tajiri kwa kubadili
fikra zako. Naamini unaendelea kufanyia kazi maarifa uliyoyapata kutoka kwenye
makala zilizotangulia ili baada ya muda tuweze kusherekea pamoja mafanikio ya
kubadili nchi hii kuwa mahala pazuri pa kuishi.
Katika makala ya leo tutaangalia jinsi
ambavyo katika maisha watu wengi wameshindwa kufikia malengo yao kwa vile wamekuwa
wakijiona kama si wahusika wakuu kwa kila jambo linalotokea maishani mwao. Tabia
hii imepelekea wahusika hawa kuwa walalamikaji pale mambo yanapokwenda kinyume
na matarajio. Wakati mwingine mtu anaanza kulalamika hata kabla hajajaribu
kufanya kile ambacho anaamini kingemtoa kimaisha.
Epuka kuwa mlalamikaji
Kwanza fikiria juu ya mafanikio ambayo
umeweza kuyapata mpaka sasa katika nyanja mbalimbali na pili jiulize ni
mikakatij/jitihada zipi ulizojiwekea wewe mwenyewe ili kufanikisha manikio
hayo. Ni dhaihiri kuwa sehemu kubwa ya ushindi wako inatokana na mikakati
unayojiwekea mwenyewe pasipo kumtegemea mtu. Kwa maana hiyo hakuna atakayekuja
kukuambia kuwa muda umefika wa wewe kutimiza ndoto zako hisipokuwa wewe
mwenyewe ndo mwenye jukumu la kuhakikisha unatimiza ndoto moja baada ya
nyingine.
Katika kufanikisha hili inahitajika nidhamu
ya hali ya juu kuhakikisha kuwa wewe unajiona kuwa ni meneja wa maisha yako
mwenyewe ili pale mambo yasipoenda sawa uwe wa kwanza kujisuta mwenyewe. Siri kubwa
iliyopo hapa ni kuwa pale unapokuwa mlalamikaji hali hii inakufanya ujitoe katika
mbio za mapambano hivyo kupelekea kusubilia muhujiza ujitokeze ili kutimiza
malengo yako. Kuanzia leo hii jione kuwa hakuna mtu au taasisi yoyote ile
inayohusika kwa njia yoyote ile katika kuwezesha kutimiza ndoto zako bali ni
wewe mwenyewe (no one to blame except yourself). Suala la ulalamikaji husilipe
tena nafasi kwani itakuwa sawa na kujilalamikia mwenyewe kwamba umeshindwa
kutimiza wajibu wako.
Mafanikio yanapatikana kwa mchakato maalamu
wenye malengo mahususi ambayo ni lazima uyafanyie kazi katika maisha yako ya
kila siku. Katika kutimiza ili naomba utambue kuwa mafanikio yanapatikana kwa
kufuata kanuni ndogondogo ulizojiwekea kwa kipindi cha muda maalumu uliojiwekea
pasipo kuvunja kanuni hizo (success is created by following simple fundamental
principles consistently overtime). Kutokana na maana hii, mafanikio ya kesho
yanatokana na kile unachokifanya kwa sasa katika kila siku ya maisha yako.
Kama utatimiza kanuni ambazo umejiwekea
itakufanya uweze kuuona ushindi katika kila iitwapo leo. Ninachomaanisha hapa ni
kwamba kanuni utakazojiwekea ili zikuwezeshe kupata utajiri kanuni hizo ni sawa
na ngazi ambazo kila siku utakuwa unapanda kutoka ngazi moja hadi nyingine. Kwa
hali hiyo itakuwa rahisi kwako kuona jinsi unavyopiga hatua tofauti na pale ambapo
husingekuwa na kanuni zozote zinazokuongoza. Kinyume chake ni kwamba mtu ambae
hana kanuni zinazomuongoza ni rahisi kukata tamaa kwa sababu atakuwa anadhani
kuwa mafanikio ni suala la siku moja.
Hitimisho
Fikiria leo hii unafanya nini ambacho
kinaweza kuwa msingi wa mafanikio yako kwa siku zijazo. Fikiria umejiwekea
kanuni zipi ambazo zitakusaidia kutimiza ndoto zako kwa muda ujao. Fikiria
mpaka sasa umepoteza fursa zipi kwa sababu tu ya kujiona kuwa mazingira
hayaridhishi jambo lilopelekea uanze kulalamikia jamii inayokuzunguka au
serikali. Mwisho malizia kwa kujisemea kuwa wewe ndo muhusika wa maisha yako na
pale utakaposhindwa kutimiza ndoto zako jisemee mwenyewe kuwa umeshindwa kwa
uzembe wako.
Kaulimbiu yangu……“FIKRI
NA UCHAGUE UTAJIRI KWA KILA ULIFANYALO”
Imeandaliwa
na Ndg.
Augustine M. Bilondwa
Karibu
kwenye fikra za kitajiri tubadilishane
mawazo kupitia mawasiliano yafuatayo:-
Namba
ya Simu ya Mkononi 0786
– 881155/0763 – 745451
Barua
pepe bilondwam@yahoo.com
Blog
fikrazakitajiri.blogspot.com