ZIJUE SHERIA HIZI ZA ASILI NA JINSI UNAVYOWEZA KUZITUMIA KUJIPATIA MAFANIKIO MAKUBWA SANA

Naamini rafiki yangu kwenye ukurasa huu upo vizuri na unaendelea kupambana ili kesho yako iwe zaidi ya leo yako hasa katika hatua zako za kujipatia mafanikio makubwa sana. 

Leo hii naomba nikushirikishe mojawapo ya sheria za asali ambazo zimekuwa zikifanya kazi katika ulimwengu huu tunamoishi kwa ajili ya kubadilisha maisha yetu ya kila siku. 

Ni wazi kuwa sheria hizi zimekuwa zikifanya kazi na hivyo kuwa na mchango mkubwa wa kuyafanya maisha yetu jinsi yalivyo pasipo sisi kujua kuwa tupo jinsi tulivyo kutokana na nguvu ya sheria hizi. Karibu uzifahamu sheria hizi ili uweze kuzitumia kujikomboa kiuchumi:
Sheria ya KUPANDA na KUVUNA (The law of Sowing and Reaping au The Law of Cause and Effect)
Sheria hii ni mojawapo ya sheria zinazobadili maisha yetu kwa kiasi kikubwa. Tupo jinsi tulivyo kutokana na msukumo wa sheria hii. Kwa ufupi ni kwamba utavuna kulingana na ulivyopanda.

Kamwe hautavuna mpunga kutoka kwenye shamba la mahindi bali ili uweze kuvuna mpunga ni lazima uwe umepanda mpunga kwenye shamba lako.

Vivyo hivyo kiasi cha mavuno kitategemea na ukubwa wa shamba lako. Kwa ufupi ni kwamba hakuna muujiza wowote ambao utakupatia kile unachotaka pasipo jitihada zako za hali na mali katika kuhakikisha kuwa unapata kile unachohitaji.
Vivyohivyo, Kama unataka kupata mafanikio makubwa sana katika maisha yako jiulize unafanya nini kwa sasa ambacho ndo mbegu unayoipanda kwa ajili ya mavuno yako hapo baadae.

Hapa namaanisha kwamba hakikisha kila unalofanya kwa leo lina mchango mkubwa kwa kesho yako hasa katika kuchangia kwenye mafanikio unayoyataka kwa maana ndoto zako ulizonazo kwa ajili ya kesho.........
Kwa leo nakuacha ukitafakali sheria hii jinsi ilivyo na mchango mkubwa kwa maisha yako jinsi yalivyo kwa sasa. Nitaendelea kukuletea sheria nyingine kwa ajili ya kukuelimisha juu ya sheria hizi.
Mathias Mgenyi Bilondwa
08786881155
onclick='window.open(