Ni matumaini yangu kuwa unaendelea
kupambana kwa ajili ya ukamilisho wa maisha yetu. Leo hii ninaendelea
kukushirikisha uchambuzi maalumu wa kitabu cha The Rules of Life ambacho kimeandikwa na mwandishi mahiri
na tajiri Richard Templar. Katika
sehemu ya awali nilikushirikisha uchambuzi wa Kanuni ya 1 hadi ya 30. Pia,
unaweza kujifunza mengi kuhusiana na kanuni za pesa kutoka kwenye kitabu chake
cha Rules
of Money.
Mwendelezo wa SEHEMU YA
KWANZA: KANUNI KWA AJILI YA NAFSI YAKO (Rules for You)
31. Kanuni ya Thelathini
na Moja: Chagua jinsi unavyotengeneza kiota chako. Mwandishi
anatushirikisha kuwa jinsi tulivyo ni matokeo ya matendo yetu ya kila siku.
Katika maneno rahisi tunaweza kusema kuwa kila mtu anavuna anachopanda,
ukipanda mbigili utavuna mbigili na vivyo hivyo ukipanda mbegu bora utavuna
mbegu bora. Matendo yako yataamua kama endapo maisha yako yatazungukwa na
furaha au huzuni. Kumbuka malipo ni hapa hapa duniani na sio kuzimu au peponi.
Mwandishi anatushirikisha kuwa wale wanaosambaza upendo na maisha yao pia
yanazungukwa na matukio ya upendo. Hivyo kutokana na kanuni hii kila mmoja wetu
ana wajibu wa kuangalia upya matendo yake.
32. Kanuni ya Thelathini
na Mbili: Wakati mwingine maisha yanaweza kuwa kama matangazo. Mwandishi
anatushirikisha kuwa pamoja na kanuni ya 31 kututaka kuwa na matendo mema kuna
nyakati ambazo utajikuta unapata kinyume na jitihada unazofanya katika matendo
yako. Hii ni sawa na kuwekeza sana kwenye matangazo ya biashara kwa ajili ya
kuongeza idadi ya wateja na badala yake unakuta ongezeko la wateja haliendani
na gharama unazoweka kwenye matangazo. Kumbe katika nyakati kama hizo si wakati
wa kukata tamaa na kufanya matendo mabaya badala yake unahitaji kuendelea
kutimiza wajibu wako wa kutenda matendo mema kwa asilimia 100. Unahitaji
kuendelea kutenda matendo mema kwani haujui ni lini utalipwa kutokana na
jitihada zako. Hapa ndipo kuna nyakati tunajiona wenye bahati kumbe si bahati
bali ndivyo tunavyolipwa kutokana na matendo yetu ambayo tunatenda na kusahau.
Kumbuka msemo wa “tenda wema na nenda zako”.
33. Kanuni ya Thelathini
na Tatu: Jifunze kutoka kwenye eneo lako la faraja (steppimg out of your
comfort zone). Kila siku jiandae kuwa mkakamavu na
jasiri katika shughuli unazofanya. Hatua hii ni muhimu kwa ajili ya kuendelea
kujenga mwili na akili kwani tunapaswa mara zote kukua kimwili na kiakili
(kiroho). Husikubali kuridhika kwani tabia ya kuridhika itakufanya upunguze jitihada
za kuutumia mwili na ubongo wako vizuri. Kuwa mtu wa kujaribu vitu vipya na
pengine visivyoonekana kuwezekana. Pia, hapa ndipo tunahitaji kuepuka imani au
tamaduni zilizopitwa na wakati ambazo zimekuwa zikituzuia kufanya vitu vipya
katika maisha yetu ya kila siku.
34. Kanuni ya Thelathini
na Nne: Jifunze kuuliza maswali. Mwandishi anatushirikisha kuwa njia bora
ya kujifunza zaidi na zaidi kupitia kuuliza maswali kuliko kujibu. Hii ni
kutokana na ukweli kwamba unapouliza swali unakuwa katika hali ya kuhitaji
kujua majibu na pale unapokuwa mtu wa kujibu maswali unajiona kujua kila kitu
na hivyo hali hiyo inadumaza ubongo wako katika kujifunza vitu vipya. Kumbe
tunapouliza mara nyingi tunakuwa katika wakati mzuri wa kuelezea hisia na
mawazo yetu katika tukio husika. Unapouliza unajiweka katika nafasi nzuri ya
kujua mawazo ya wengine na hivyo kupata nafasi ya kutoa mawazo yako kwa mantiki
(logic), upole na usahihi. Jiulize mwenyewe kwa nini unafanya kile unachofanya
au kwa nini unahisi upo sahihi au kwa nini unahisi sio sahihi.
35. Kanuni ya Thelathini na Tano: Kuwa na Heshima. Mwandishi
anatushirikisha kuwa watu wengi waliofanikiwa kwa maana ya kuishi maisha ya
amani, upendo, kuridhika na furaha ni wale ambao wameishi maisha ya kawaida na
heshima kwa watu wote. Watu hawa hawapendi kutangaza umaarufu au uwezo wao
kwani muda wote wanajiona hawana kitu cha thamani au hawapo tofauti na jamii
inayowazunguka. Hivyo katika kanuni hii tunafundishwa kuishi maisha ya kawaida
na upole bila kujali ni mafanikio kiasi gani tumejaliwa.
36. Kanuni ya Thelathini na Sita: Ni sahihi kuwa na hisia kali. Mwandishi
anatushirikisha kuwa sisi ni binadamu na hivyo ni sahihi kuwa na hisia kali
pale inapobidi. Kama umekasirishwa ni sahihi kuwa na hisia za hasira; kama
umeondokewa na mpendwa au mtu wa karibu ni sahihi kuwa na hisia za
huzuni/majonzi; kama kuna tukio limekufurahisha ni sahihi kuwa na hisia zaidi
za furaha; ni sahihi kuwa na
hofu, wasiwasi, msisimko, wasiwasi, na kila aina ya hisia. Vivyo hivyo
hatupaswi kuficha hisia zetu kwa kuogopa kuwa watu watatuona vipi. Hata hivyo
tunahitaji kukumbuka kuwa hisia zote hizi zinatakiwa kuonyeshwa kulingana na
matukio ambayo tunakumbana nayo katika maisha ya kila siku. Pamoja na hisia
zote hizo tunakiwa kuwa na uwezo wa kudhibiti hisia zetu ili zisije kusababisha
madhara zaidi.
37. Kanuni ya Thelathini na Saba: Linda imani yako. Kulinda
imani yako ni kulinda zile ahadi ulizojiwekea ili kuendelea kuishi katika misingi
uliyojiwekea kwenye kila sekta ya maisha yako. Hii ni pamoja na kujilinda dhidi
ya kiburi, majivuno, chuki, wivu na kuendelea kujitoa kwa ajili wale
wanaohitaji msaada wako wa kila aina. Mwandishi anatushirikisha kuwa pamoja na
yote hatupaswi kushawishi watu wengine kuamini katika misingi tunayoishi bali
matendo na mwonekano wetu ndo vitutambulishe zaidi (kumbuka kanuni ya kwanza –
ifanye iwe siri yako).
38. Kanuni ya Thelathini na Nane: Kamwe hakuna siku utafahamu kila
kitu. Mwandishi anatushirikisha kuwa sisi ni chembe tu ya
viumbe katika ulimwengu huu wenye mambo mengi na magumu kueleweka katika kila
sekta ya maisha yetu. Kwa kutambua kanuni hii kumbe tunapaswa kuwa na usingizi
bora usiku kuliko kuumiza kichwa kuwa jambo fulani halipo kwenye upeo wetu. Ni
kutokana na kanuni hii tutegemee baadhi ya mambo kwenda kinyume kuliko
matarajio yetu, vivyo hivyo, tutegemee baadhi ya watu kutenda matukio yasiyo
rafiki dhidi yetu. Kumbe kwa kutambua kanuni hii, hayo yote hayapaswi kukuumiza
bali yakupe mwanga wa kuendelea na maisha kama kawaida. Muhimu ni kutambua kuwa
kwa sasa tunaishi katika ulimwengu wa taarifa kuliko kipindi chochote kile,
hivyo unaweza kujifunza mambo mengi yanayokutatiza hata ukiwa umejifungia
chumbani kwako. Kanuni hii inakupa nafasi ya kutambua kuwa dunia ina mambo
mengi na sio lazima yote uyafahamu – chambua machache muhimu kwako na
kuyafanyia kazi.
39. Kanuni ya Thelathini na Tisa: Tambua furaha yako ya kweli
inatoka wapi. Mwandishi anatushirikisha kuwa furaha ya
kweli kwa mwanadamu ni kitendawili ambacho wanafalsafa wengi wanaangaika
kukitegua. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kile kinachokupa furaha yawezekana
sio kile kinachonipa furaha. Na pengine furaha hii inakuwa ni ya muda tu kwa
vile mwanadamu ameumbwa katika hali ya kutokuridhika. Kumbe unahitaji kufahamu
ni kipi chanzo halisi cha furaha yako. Kama ni mpenzi wako, nyumba, gari,
ufahari au watoto hakikisha unatambua ni kipi hasa ndani ya hivyo vyote
kinachopelekea kuwa na furaha tena furaha ya kudumu. Mwisho mwandishi anatushirikisha
kuwa siri kubwa ya kuwa na furaha ya kweli ni kutambua chanzo halisi cha furaha
yako na namna ya kuichochea/kuianzisha mwenyewe bila kusubiria mazingira ya
kutoka nje ya nafsi yako.
40. Kanuni ya Arobaini: Maisha ni sawa na Pizza. Mwanidishi
anatushirikisha kuwa maisha ni sawa na Pizza na kama kawaida pamoja na utamu
wake Pizza kuna nyakati ambazo inakuwa na viungo ambavyo si rafiki kwako kwa
maana huvipendi. Ndivyo maisha yalivyo kwa kuwa yana mchanganyiko wa kila kitu.
Katika maisha kuna vitu vingi vizuri japo pia kuna vitu vingi vya hovyo, hivyo
kutokana na kanuni hii tunahitaji kuchagua mazuri katika maisha na kuachana na
yale mabaya. Mfano, kama unampenda sana mwenzi wako japo ana tabia ya kuwa na
jazba mnapokuwa kwenye majibizano basi endelea kumpenda zaidi huku ukitafuta
njia bora ya kuongea nae bila ya kuwa na jazba. Kanuni hii inatukumbusha kuwa
kamwe hautapata ukamilifu wa asilimia mia katika kile unachokipenda. Ni
kutokana na ukweli huo tunahitaji kutafuta mazuri katika matukio ya maisha yetu
ya kila siku na kuyafanyia kazi huku tukijifunza kukabiliana na mabaya.
41. Kanuni ya Arobaini na moja ------ 102. Kanuni ya mia na mbili:
Pata uchambuzi wa kanuni zote 106 na kwa
kuchangia Tshs. 5000/= tu.
103. Kanuni ya Mia na Tatu: Angalia
historia itaandika nini kuhusu wewe. Tunafahamu
kabisa kuwa duniani hapa sisi sote ni maua ambayo yanachanua kwa muda mfupi na
hatimaye hunyauka. Katika kipindi hicho cha muda mfupi ambacho tumejaliwa
kuishi ni lazima tujiulize historia itaandika nini dhidi kwa ajili ya vizazi
vijavyo. Kumbe kila siku tunahitaji kujiuliza swali hili “ikitokea nimekufa leo – watu
watasema nini kwenye mazishi na matanga ya msiba wangu”? Je nimetenda mema
kuliko maovu au kinyume chake ni sahihi? Kanuni hii inatutaka
kuhakikisha tunajihusisha na mambo ambayo hakika yataweka alama kwenye uso wa
dunia hii ili siku ambayo maisha yetu yatafikia ukomo alama hizo ziendelee
kukumbukwa vizazi na vizazi kama sehemu ya kuenzi muda mfupi ambao tumebahatika
kuishi. Kumbuka tuna wajibu mkubwa wa kuhakikisha tunaifanya dunia hii kuwa
mahala pazuri pa kuishi ili kizazi kinachokuja kirithi mazingira safi na salama
kuliko jinsi tulivyoyakuta. Kumbe, mara zote tunahitaji kuogopa laana za vizazi
vijavyo ambazo zitatokana na vizazi hivi kurithishwa dunia ambayo ina kila aina
ya uovu, mateso na manyanyaso yaliyosababishwa na uharibifu wa mazingira pamoja
na mmomonyoko wa maadili.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Waoooooh….. najisikia
amani na furaha kuona nimesoma kitabu hiki mwanzo mwisho na hivyo nimebahatika
kusoma kanuni zote 106. Najisikia amani moyoni kuona kuwa kazi hii nimeifanya
kwa weledi kwa kadri ya uwezo wangu na hatimaye nimefanikiwa kukuchambulia
kanuni zote 106 kwa lugha yenye misamihati rahisi. Kubwa zaidi nitajisikia
amani zaidi na zaidi kuliko niliyonayo sasa endapo uchambuzi huu utasomwa kwa
ufasaha na watu wasiopungua 1,000. Naamini watu 1,000 wakisoma uchambuzi huu ni
kila mmoja kuchukua kanuni zisizopungua 10; Watu hawa watagusa maisha ya watu
zaidi ya milioni kumi (10,000,000).
Mlengwa nambari moja ni wewe ambaye umesoma
baadhi ya kanuni hizi. Kwa kuwa umeweza kusoma japo kwa kiasi ni matumaini
yangu kuwa na wewe ni mtafutaji kama mimi ambaye umedhamiria kufanya kitu kwa
ajili ya maisha yako na jamii inayokuzunguka. Je historia itaandika nini kuhusu
wewe kwa muda mfupi ambao umebahatika kuishi hapa duniani? Nisaidie kusambaza
upendo ambao mimi nimekufikishia kupitia uchambuzi wa kitabu hiki.
Kanuni hizi zote zimejumuisha sekta zote
maisha ambazo zinajumuisha: (a) Kanuni kukuhusu wewe binafsi (Kanuni ya 1 hadi
56); (b) Kanuni za Mahusiano na Mwenza wako (Kanuni ya 57 hadi 72); (c) Kanuni
kwa ajili ya familia na marafiki (Kanuni ya 73 hadi 86); na (d) Kanuni za
kijamii na mazingira (86 hadi 106). Uchambuzi huu si wa kukosa kama unahitaji
kubadilisha maisha yako.
Lipia TSHS. 5,000/= kwa
ajili ya kupata uchambuzi wa kina wa kanuni zote (106) ambao umeandaliwa kwa
mfumo wa pdf. Uchambuzi huu una jumla ya kurasa 40 na ni kitabu ambacho unaweza
kusoma kwenye simu yako ya mkononi (smart phone) au kwenye kompyuta mpakato
(pc).
Kupata uchambuzi wa
kanuni zote tuma pesa yako kwa njia ya M-pesa au Airtel Money kupitia namba
zifuatazo:-
M – Pesa tumia namba:
0763 745 451 (Majina ni Augustine Mathias)
Airtel Money tumia namba:
0786 881 151 451 (Majina ni Augustine Mathias)
Baada kutuma pesa hiyo
nitumie ujumbe kwenye namba ya airtel (0786 881 151 451) ukiwa na barua pepe
yako ili nikutumie uchambuzi wa kanuni hizi moja kwa moja kwenye barua pepe
yako.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Pia unaweza kupata
uchambuzi wa Kitabu cha “The Rules of
Money” ambacho pia kimeandikwa na Mwandishi Richard Templar.
Uchambuzi wa kina wa Kitabu cha The Rules of Money (Kanuni 107)
umeandaliwa kwa mfumo wa pdf na unapatikana kwa gharama ya Shilingi za
Kitanzania (TSHS) elfu tano tu (5,000/=). Uchambuzi wa kanuni zote una jumla ya
kurasa 39.
Kupata uchambuzi wa kanuni zote tuma pesa yako kwa njia ya M-pesa
au Airtel Money kupitia namba zifuatazo:-
M – Pesa tumia namba: 0763 745 451 (Majina ni Augustine Mathias)
Airtel Money tumia namba: 0786 881 151 451 (Majina ni Augustine
Mathias)
Baada kutuma pesa hiyo nitumie ujumbe kwenye namba ya airtel (0786
881 151 451) ukiwa na barua pepe yako ili nikutumie uchambuzi wa kanuni hizi
moja kwa moja kwenye mtandao wako.
Karibu kwenye mtandao wa FIKRA ZA KITAJIRI ili upate elimu isiyokuwa na mwisho.
Born to Win ~ Dream Big
Augustine Mathias Bilondwa
Namba ya Simu: 0786881155
Mwanzilishi wa Mtandao wa fikrazakitajiri.blogspot.com
Barua pepe: fikrazatajiri@gmail.com
Ukurasa wa facebook: Fikra za Kitajiri: Fikri na Kutenda Kitajiri: Elimika na Tajirika