SHERIA YA KUTOA NA KUPOKEA (the law of giving and receiving)
Karibu rafiki yangu kwenye ukurasa huu kwa ajili ya mwendelezo wa SHERIA za asili na jinsi tunavyoweza kuzitumia kufikia mafanikio makubwa sana katika maisha yetu. Katika sehemu ya kwanza tuliona juu ya SHERIA ya kupanda na kuvuna na jinsi ilivyo na nguvu kubwa katika maisha yetu kwa maana ya kwamba tupo jinsi tulivyo kutokanà na kile ambacho tumekuwa tukipanda (tunavuna kutokana na kile tunachokipanda). Vivyohivyo katika sehemu ya pili tuliona nguvu ya SHERIA ya asili ya uotaji (the law of germination) tunavyoweza kuitumia kufikia mafanikio makubwa sana. Kama hukubahatika kusoma juu ya SHERIA hizo mbili nakushauri uzipitie kabla ya kuendelea na SHERIA hii ya sehemu ya tatu.
Leo hii naomba tuangalie nguvu iliyopo kwenye SHERIA ya asili ya kutoa na kupokea katika maisha yetu ya kila siku. SHERIA hii ya asili inasema kuwa tunapokea kwa kadri tunavyokuwa wepesi wa kutoa. Kwa kifupi ni kwamba hakuna kitu chochote kinachopatikana pasipokuwepo utayari wetu wa kutoa kwanza sehemu ya kile tulichonacho. Pia tunakumbushwa kuwa pale tunapotoa hatutakiwi kutoa kwa makusudio ya kwamba tunatoa ili kupata siku Fulani bali tunapotoa tutoe kwa roho moja tukijua kuwa pale tulipotoa lazima nguvu ya uwiano (equilibrium) itatumika kurejesha mzani kwenye hali yake ya awali.
Hapa unaweza kujiuliza kuwa mbona huwa ninapokea pasipo kutoa? Rafiki hilo ni swali ambalo wengi wetu tunaweza kujiuliza Mara baada ya kuijua sheria hii. Jibu ni kwamba tumekuwa tukitoa pasipo sisi kujua na ndo maana tumeendelea kupata yale tunayopokea kwa sasa. Hata hivyo yawezekana tumeendelea kupokea kidogo kwa vile na sisi hatutumii sheria hii ya asili ipasavyo.
Kuanzia sasa ijaribu sheria hii ya asili ili uendelee kupokea kwa uwiano sawa. Itumie sheria hii kwa kutoa physically na emotionally. Waweza kutoa kwa njia vitu ulivyonavyo kwa kadri uonavyo inafaa au waweza kutoa kwa njia ya vipaji ulivyojaliwa kama kutoa ushauri, kuelimisha n.k
Kama umejifunza kitu kupitia ujumbe huu mshrikishe na mwanzako ili elimu hii iwafikie wengi kwa kadri iwezekanvyo....
A.M.Bilondwam
bilondwam@gmail.com
0786 881155
bilondwam@gmail.com
0786 881155