ZIJUE SHERIA ZA ASILI NA JINSI YA KUZITUMIA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA SANA - SEHEMU YA NNE

SHERIA YA UWILI KINZANI (THE LAW OF POLARITY)

Ni muda mwingine rafiki nakuletea mfululizo wa elimu juu ya sheria za asili na jinsi ambavyo tunaweza kuzitumia kufikia mafanikio makubwa sana. Ni matumani yangu kuwa upo vizuri na unaendelea kupigana ili uweze kutimiza ndoto zako. 

Hongera sana rafiki kwa kuendelea kulisukuma gurudumu hilo  ambalo kuna makorongo na milima mingi ambayo inabidi uipitie ili hatimaye ufanikiwe. Nasema haya kwani naamini rafiki yangu una ndoto ambazo ungependa siku moja uweze kuzitimiza, kama ndo hivyo hongera sana rafiki kwani maisha bila ndoto ni sawa na kwamba muhusika tayari hana maisha (life without viable dreams is a dead end).

Karibu rafiki katika mfululizo wa ufahamu wetu kwenye sheria za asili ambalo Leo hii ningependa nikushirkishe juu ya sheria ya uwili kinzani na mchango wake katika maisha yetu ya kila siku. 

Sheria hii imekuwepo toka kuumbwa kwa dunia na imekuwa na nguvu kubwa katika kubadilisha maisha ya watu na imekuwa na mchango mkubwa kwa waliofanikiwa sana katika maisha yao. Sheria hii inasema kuwa kila jambo/hali iliyopo hapa duniani inapatikana katika hali ya uwili unaokinzani. 

Mfano, kama kuna juu pia kuna chini, kama kuna kushindwa pia kuna kushinda, kama kuna furaha pia kuna huzuni, kama kuna nje pia kuna ndani, kama kuna mchana pia kuna usiku, kama kuna mwanga pia kuna giza, kama kuna tajiri kuna masikini pia........

Kwa ujumla ni kwamba sheria hii inatuambia kila hali/fursa tunaweza kuitazama katika sura mbili upande chanya au upande hasi. Watu wengi wameshindwa kufikia mafanikio makubwa kwa vile wamekuwa wakiangalia upande mmoja kwenye fursha/hali wanazokutana nazo. 

Mfano, badala ya kujingea nidhamu ya kufikiri katika hali chanya watu wengi wamekuwa wakifikiri katika hali hasi. Watu wengi wameshindwa kuchangamkia fursa nyingi kwa kile kinachoitwa hofu ya kushindwa au kupoteza kile walichonacho endapo watajaribu kuchangamkia fursa husika. 

Watu wengi wameendelea kuamini kuwa mafanikio ya kifedha (financial freedom) ni kwa wateule wachache waliobarikiwa. Yapo mengi ambayo naweza kukutolea mfano juu ya jinsi gani ambavyo watu wamekuwa wakishindwa kufikia mafanikio makubwa sana kutokana na kutokujua nguvu ya sheria hii na hivyo kupelekea kuharibu maisha yao pasipo wao kujua kuwa wao ndo chanzo cha jinsi maisha yao yalivyo.

MUHIMU: Kuanzia sasa hakikisha unaifundusha akili kusimama katika upande wenye manufaa kwa ajili ya kesho yako. Achana kabisa na upande hasi ambao unapelekea wewe kupoteza fursa nyingi kila iitwapo leo. Tafakari ni jinsi gani umekorofishana na wenzako au umeshindwa kuchangamkia fursa nyingi kwa kile ambacho sheria hii inatuambia kuwa ni kuangali vitu/hali kwa upande mmoja. Tumia sheria hii kujua kuwa wewe ndo dereva namba moja wa maisha yako wala si Serikali, mzazi wala ndugu jamaa na marafiki.

Kama umejifunza kitu naomba uwashirikishe wale uwapendao kwa ajili ya kusambaza elimu hii kwa watu wengi na hatimaye tufanikiwe kuifanya dunia hii kuwa mahala pazuri pa kuishi.

THINK AND TAKE ACTION RIGHT NOW
A.M. BILONDWA
0786881155
bilondwam@yahoo.com
onclick='window.open(